‘Sichame Ago

Hamad Hamad Machi 10, 2011 Copenhagen

Sichami ago hanyela, nacha kuja wiya papo
Senda mbali hazurura, hasahau niwiyako
Taenzi ago kabula, sijafikwa ni mafiko
Tatukanaje wavyele, na uzazi ungalipo?

Sitacha m’bacha wangu, kwa mswala wa kupita
Habeza na walo wangu, waloniendesha tata
Wao ndio myega yangu, myengine sitaipata
Nshafunzwa n’mamangu, ‘limwengu haunipata Continue reading “‘Sichame Ago”