Nayacha macho ya wachwa, pale zama yachunzapo
Nayacha kucha na kuchwa, yachecheapo nilipo
Nayo yakijua yachwa, ndo uchunzi uzidipo
Nacha sitachapo kucha, yachwayo nami nayacha Continue reading “Nacha”
Month: May 2011
Nazingwa
Nazingwa ni ndugu zangu, wasonijua nilipo
Waumia kwa uchungu, kila wanikumbukapo
Waniombea kwa Mungu, mafanikio na pepo
Numonumo ndilo langu, tenda, tarudia kuko. Continue reading “Nazingwa”
Hunifai
Wanitaka niwe wako, ati wa ubani
Niwe wako mali yako, niwewo mwandani
Siliwezi penzi lako, sebu abadani
Bora kaa peke yako, uwe mbali nami Continue reading “Hunifai”
Ni Lipi Kosa Langu?
Karima ni Mola wangu, uwezo kunijalia
Huu si uwezo wangu, kipaji kutunikiwa
Kutupa kalamu yangu, hekima kuwapatia
Ni lipi kosa langu, dharau kutunikiwa? Continue reading “Ni Lipi Kosa Langu?”
Hamkani
Dhoruba hii hakika, huchukua na kuzoa
Kwa wenye kubahatika, na kwa kipaji Jalia
Seuze wa tikatika, na wale mazoa zoa
Nani atabakia? Continue reading “Hamkani”
Salata
Uliniahidi, kwamba wenipenda ‘tanitumikia
Ukaitakidi, kuwa ‘tanilinda na kunitetea
Iwapi ahadi, mbona kushapinda wanigeukia? Continue reading “Salata”
Kata’ani
Haiwi!
Na wala haitokuwa
Kata’ani nakataa
Kuonewa!
Kubugudhiwa!
Kusulubiwa!
Kamwe haitokuwa Continue reading “Kata’ani”