Kake njo’vyo nyumbani, uje uone rahaye
Uje wende forodhani, na shamba utembeleye
Usikie waadhini, mbio uwakimbiliye
Bi mama akutamani, na wana usikisiye
Njoo kake njoo, njoo ututembeleye Continue reading “Kake Njoo Nyumbani”
Month: June 2011
Nataka Nende Nyumbani
Nataka nende nyumbani, haone wangu wavyele
Haanze walo Ziwani, Shengejuu hadi Ole
Hashibishe zao mboni, nami moyo utulile
Mola wangu niauni, lengo langu nifikile Continue reading “Nataka Nende Nyumbani”
Utamu Wake Shairi – Jawabu 1
Kwa jinalo Rahmani, Mola wetu Msifika
Naomba uniauni, kwa hili ninalotaka
Naingia utungoni, mchango wangu kuweka
Unipe njema lisani, mazuri kuyatamka Continue reading “Utamu Wake Shairi – Jawabu 1”
Utamu Wake Shairi (Suali)
Nataka uliza swali, kuwauliza malenga
Wa karibu na wa mbali, wakomavu na wachanga
Musemao Kiswahili, kiarabu na kimanga
Ipi tamu ya shairi, tungoni inovutiya? Continue reading “Utamu Wake Shairi (Suali)”