Herufi na Sauti za Kiswahili

Kiswahili kilipoanza kurikodiwa kimaandishi hakikuwa kikiandikwa kwa herufi hizi zinazoitwa za Kilatini, bali kwa zile za Kiarabu. Kwa mtazamo wangu, miongoni mwa misiba mikuu iliyokikumba Kiswahili ni huu wa kubadilishwa herufi zake mwanzoni mwa karne ya 19 baada ya upwa wa Afrika Mashariki kuvamiwa na Wazungu wakoloni. Continue reading “Herufi na Sauti za Kiswahili”

Vitenzi Vitatu: Kuwa, Kuwako na Kuwa na

Kiswahili kina vitenzi hivi vitatu, ambavyo licha ya kuwa na maumbile yanayokaribiana, vina maana tafauti. Vitenzi hivyo ni kuwa, kuwako na kuwa na. Hiki kitenzi kuwako kinaweza pia kuandikwa kuwapo au kuwamo kwa mujibu wa muktadha unaohusika; lakini hiyo si mada kwa leo. Mada ni kuangalia mgusano na muachano wa vitenzi hivi vitatu vya kuwa, kuwako na kuwa na. Continue reading “Vitenzi Vitatu: Kuwa, Kuwako na Kuwa na”

Majina yenye wingi na au kundi zaidi ya moja

Kuna idadi isiyo ndogo ya majina kwenye Kiswahili ambayo huchukua maumbile na makundi tafauti. Miongoni mwa sababu ni kuwa aidha majina hayo yanawakilisha maana tafauti licha ya kuwa na umbile moja, ama ni majina yanayofanana kwa herufi zake lakini tafauti kwenye matamshi na hivyo makundi na, au, ni majina yanayowakilisha dhana moja lakini kwa viwango tafauti. Mada ya leo inazungumzia suala hilo. Continue reading “Majina yenye wingi na au kundi zaidi ya moja”

Yaliyomo kwenye kundi la YU-A-WA

Sadfa imeyaweka majina yanayonasibishwa na roho (nafsi) kwenye kundi la YU-A-WA, vikiwemo viumbe tunavyoviona – watu, wanyama, ndege na samaki – hadi tunavyoamini kuwapo kwake bila kuviona kama malaika, majini, mashetani au pepo. Wote hao wanaingia kwenye kundi hili. Sadfa pia imefanya hili liwe kundi pekee ambalo hayakutikani majina yasiyo na sifa ya nafsi. Continue reading “Yaliyomo kwenye kundi la YU-A-WA”

Kundi la I-ZI: Urahisi na ugumu wake

Kama katika makala iliyotangulia, ninasisitiza tena unasibu katika lugha, sifa ambayo ni ya jumla kwa kila lugha na sio Kiswahili pekee. Mpwa wangu, Khelef Nassor, ameifafanua vyema zaidi dhana hii katika mchango wake kwenye mada iliyopita. Leo tuzungumzie kundi la majina la I-ZI, msisitizo ukiwa urahisi na kile kinachoweza kuitwa ‘ugumu’ wake. Hii nukta ya ugumu ninaiwekea alama makusudi, maana inahojika zaidi. Continue reading “Kundi la I-ZI: Urahisi na ugumu wake”