Kwa Jinalo Zanzibari

Kwa jina la Zanzibari, uhuru tuliupata
Uhuru ulobashiri, Zanzibar kuneemeka
Mwezi wa kumi na mbili, sitini na tatu mwaka
Na UN tukafika

Kwa jina la Zanzibari, uhuru tukaja pokwa
Mapinduzi Januari, ndicho kilichofanyika
Tukanza upya safari, kwenda tusikokutaka
Tukaanza taabika

Kwa jina la Zanzibari, mapinduzi yakatekwa
Kwa mungano uso kheri, Unguja na Tanganyika
Tukawa kama sifuri, nchi iso mamlaka
Ndipo hapa tupo sasa Continue reading “Kwa Jinalo Zanzibari”