Makala hii inajaribu kuuliza swali hili: Je, mitandao ya idhaa za Kiswahili za redio za kimataifa zina wajibu kwenye ujengaji wa Kiswahili Sanifu. Si makala yenye majibu, bali inayotaka tu kulifafanua swali lenyewe ili watafiti waje na majibu. Continue reading “Idhaa za kimataifa na Kiswahili Sanifu”
Month: March 2014
‘Kiasi ya….’ ama ‘kiasi cha…’?
Kila lugha ina kanuni zake zinazoiongoza na kwa hakika ndio misingi ambayo kwayo lugha hiyo husimamia. Katika ujumla wake, kanuni hizo huitwa sarufi, lakini katika uchambuzi wake, taaluma ya sayansi za lugha, isimu, hukichambua kila kiwango na kipenu cha sarufi kwa mawanda na vina vyake. Ndiyo maana ilimu ikaitwa ilimu, kwa kuwa huzama na kujichawanya. Continue reading “‘Kiasi ya….’ ama ‘kiasi cha…’?”
Yatwawa
Yatwawa nchi yatwawa, waichukua wenyewe
Yatwawa mbele kifuwa, kwa shangwe na kwa mayowe
Wenyewe waichukuwa, wainyakuwa ja mwewe
Na kwao yasubiriwa, yende ikapokelewe