Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini

Tukichunguza hazina ya uhakiki uliofanywa katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili na kuiweka katika mizani, upande mmoja ubebe tahakiki zilizozingatia maudhui na mwingine zile zilizoangaza fani, upande wa maudhui utalemewa na uzito na kuanguka. Ni kweli kuwa umuhimu wa fasihi katika jamii unatokana na jinsi ambavyo inaimulika jamii na kuichora kwa madhumuni ya kuihakiki na kuirekebisha kutokana na udhati na uzito wa mafunzo mwafaka inayoyabeba. Ni kweli vile vile kuwa fasihi ni sanaa kutokana na matumizi ya pekee ya lugha na vipengele vingine vya fani ambavyo kwa pamoja huipa sura maalum na kuyafanya maudhui yake yatufikie katika hali na umbo linalovutia. Hali hii ndiyo huiwezesha fasihi kutuingia, ikatuchoma na kutufikirisha zaidi. Ndio nguzo ya utamu wa fasihi.

Continue reading “Usimulizi wa Riwaya ya Nyongo Mkalia Ini”

Sitiari za ‘Mzee wa Kimbunga’

Ushairi ni mchezo. Mchezo wa maneno na hisia za watu. Katika makala haya nataka nieleze machache kuhusu tungo za Mzee Haji Gora Haji anayejulikana pia kwa jina la ‘Mzee Kimbunga’ kutokana na jina la kitabu chake kilichopigwa chapa na kutolewa 1994. Nataka kutoa mifano michache ya sitiari anazozitumia, vipi zinavyohusiana na ‘fikra kuu hiyo inayoshikiliwa na kusisitizwa’ na yeye mwenyewe anatambulika kama mtu gani. Continue reading “Sitiari za ‘Mzee wa Kimbunga’”

Vuta N’Kuvute ya Shafi Adam Shafi

Kwa miongo mingi sasa, wahakiki wa kazi za fasihi wamezisifu kazi za waandishi wa Kizanzibari kwa sifa tele. Kwa mfano, akirejea riwaya za Mohamed Suleiman Mohamed, Said Ahmed Mohamed na Shafi Adam Shafi, M. M. Mulokozi aliandika mwaka 1985: “Maendeleo muhimu kabisa, na pengine ya kufurahisha sana, katika kazi za fasihi za Kiswahili katika miaka ya 1970 na 1980, ni kuibuka kwa Zanzibar kama mtoaji bora kabisa wa kazi za Kiswahili kuwahi kutokea hadi sasa, na kiongozi wa wazi wa riwaya za Kiswahili katika siku zijazo.” Continue reading “Vuta N’Kuvute ya Shafi Adam Shafi”

‘Karamu’ ya Jumba Maro na chaguzi barani Afrika

Kwa vile Jumba Maro si riwaya yenye hadithi moja refu, bali mkusanyiko wa hadithi nyingi fupi fupi, tutachambua moja tu kati ya hadithi 12 zilizomo, tukiamini kuwa itatusaidia kuuona undani wa ‘Jumba’ lote.   Hadithi iliyopewa jina la Karamu, kama zilivyo nyingine, inaanza na ushairi uitwao ‘Mjumbe Kaemewa’. Continue reading “‘Karamu’ ya Jumba Maro na chaguzi barani Afrika”