Unasibu kwenye YU-A-WA

Wananadharia wa lugha wanakubaliana kwamba lugha ni sauti za nasibu, yaani sauti za kubahatisha. Kwa mfano, ni suala la sadfa tu kwamba sauti ‘e’ ikichanganywa na ‘mbe’ inakuwa ’embe’, mojawapo ya matunda matamu ya nchi za joto. Kwa mantiki hiyo, hakuna chochote – nje ya unasibu – zilizofanya sauti hizo zikusanyike pamoja na kutoa neno la lugha linalowakilisha tunda hilo. Continue reading “Unasibu kwenye YU-A-WA”