Dunia kokwa ya furu: Amali ya Misemo ya KiPemba

Jitihada za ukusanyaji na uchambuzi wa data za kifoklo za launi za Kipemba si jambo geni (angalia Whiteley (1958) na Mlacha (1995:21-25). Lakini kadri, muda unavyopita jitihada hizo zinaelekea kupungua kasi. Suala la uhifadhi wa ‘bohari la hekima ya wahenga wetu kimaandishi’ ni la wajibu na halipaswi kusita. Katika mradi huu unaoendelea, tumeonelea kufanya mambo mawili makuu (a) kuorodhesha na kujadili data za kifoklo zenye kuweka wazi umahususi wa launi za Kipemba. (b) Kuorodhesha na kuchambua kiethnografia data hizo kwa mujibu wa mtazamo wa uchambuzi wa data za kifoklo kimuktadha (Hymes (1962).

Makala ya Ahmad Kipacha na Ibun Kombo wa Chuo Kikuu cha Dodoma iliyochapishwa kwa mara ya kwanza na Journal of Humanities, Toleo Na. 1 la mwaka 2009. Continue reading “Dunia kokwa ya furu: Amali ya Misemo ya KiPemba”

Uhusiano baina ya Kimakunduchi na Kiswahili Sanifu

Kumekuwa na mjadala mrefu miongoni mwa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ikiwa kile kichachoitwa Kiswahili Sanifu ni lugha kamili na tafauti na lugha nyengine zinazozungumzwa kwenye maeneo yanayopakana nacho, kama vile Kimakunduchi (au Kikaye) kinachozungumzwa kusini mwa kisiwa cha Unguja, au zote kwa pamoja ni lahaja za lugha moja kuu, yaani Kiswahili. Msikilize Dk. Hans Mussa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichambua tafauti baina ya Kimakunduchi na Kiswahili Sanifu mbele ya hadhara ya Kongamano la 29 la Kiswahili la Bayreuth, kusini mwa Ujerumani. Continue reading “Uhusiano baina ya Kimakunduchi na Kiswahili Sanifu”

Sitiari katika kazi za fasihi

Wataalamu na wachambuzi wa fasihi wanakipa umuhimu mkubwa kipengele cha sitiari (uhamishaji wa sifa kutoka kitu kimoja kwenda chengine) miongoni mwa tamathali za semi katika fasihi. Kuna ambao wanafikia umbali wa kuhoji kuwa ni kipengele hiki pekee ambacho kinaweza kuipa uhai kazi ya fasihi na kuifanya isimame kwenye maana halisi. Sikiliza hapa mhadhara wa Profesa Kulikoyela Kahigi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mbele ya Kongamano la 29 la Kiswahili la Bayreuth, kusini mwa Ujerumani.  Continue reading “Sitiari katika kazi za fasihi”

Utani miongoni mwa Waswahili wa Zanzibar

Kuna pande mbili za mitazamo kuhusiana na asili ya Wazanzibari: wapo wanaodai kuwa Wazanzibari ni mchanganyiko wa watu wa makabila tofauti kutoka ile iliyokuja kuitwa baadaye Tanganyika na kisha Tanzania Bara – kama vile Bagamoyo, Tanga, Kunduchi na kwengineko. Continue reading “Utani miongoni mwa Waswahili wa Zanzibar”