Kurasa Mpya: Fungamano la Malenga

Ushairi unatambuliwa kuwa miongoni mwa sanaa kongwe kabisa kwa mwanaadamu. Jamii yoyote inayojitambuwa kwa ukale na ukongwe wake, basi utaikuta ndani yake ikiwa na sanaa ya ushairi kama moja ya dalili za uwepo wake wa zama na zama. Haitoshi hayo, ushairi pia unachukuliwa na wasomi wa taaluma za kibinaadamu, kuwa moja ya nguzo kuu za ilimu ya falsafa. Kwa ujumla, fasihi – ambayo yenyewe ndiyo mama wa maarifa ya mwanaadamu – inabebwa na tanzu nyingi, na kongwe yao ni ushairi. Continue reading “Kurasa Mpya: Fungamano la Malenga”

Kalamu ya Mapinduzi: Mapambano Yanaendelea

Ni jambo gumu kuyazungumzia maandishi bila ya kumgusa mwandishi wake, khasa pale maandishi yenyewe yanapokugusa na kuchoma mithali ya hivi zilivyo tungo za Kalamu ya Mapinduzi na unapokuwa unamfahamu mwandishi binafsi. Continue reading “Kalamu ya Mapinduzi: Mapambano Yanaendelea”

N’na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini

Siku ilikuwa Jumatano. Tarehe ilikuwa 1 Septemba 2010. Majira yalikuwa ya saa 4:00 usiku. Mahala palikuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam, mji mkuu wa kibiashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nakumbuka kila kitu kuhusu siku hiyo. Nikiwa kwenye sehemu ya kusafiria abiria waitwao wa kimataifa, nilitoa simu yangu ya mkononi nikawasiliana na watu kadhaa kwa nia ya kuwaaga. Kati yao ni mama zangu wawili, aliyenizaa Abeida bint Nassor na aliyenilea Salama bint Said, mke wangu Tauhida bint Mkwale na dada yangu Fatma bint Khelef. Continue reading “N’na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini”