Nimetangulia kusema kwamba hayo niliyoyaeleza kabla hayakuwa yamenishughulisha sana kwa sababu, mtu aweza kuwa na hiari ya kutumia maneno kandarasi/makandarasi au mkandarasi/wakandarasi, akusudiapo kuwa ni mtu. (Mimi nitaendelea kutumia kandarasi/makandarasi – tena bila ya wasiwasi wowote!) Continue reading “Baina ya mkandarasi na kandarasi – 2”
Category: Darasani kwa Mwalimu Abdilatif
Ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya lugha unaofanywa na mwalimu wa muda mrefu wa lugha ya Kiswahili, Abdilatif Abdalla.
Baina ya mkandarasi na kandarasi
Mmojawapo miongoni mwa washairi maarufu wa Tanzania, Khamis Amani Nyamaume (1926-1971), katika shairi lake labeti nne, liitwalo ‘Saa’, alitunga akasema:
Saa za huku na huko, zimekosana majira
Sababu ni mzunguko, haufuati duara
Sasa rai iliyoko, ni kubadilisha dira
Saa zatupa majira, mafundi zitengezeni… Continue reading “Baina ya mkandarasi na kandarasi”
Wapi neno mwanana hutumika?

Juza, juvya, na julisha

Neno “juvya” si ‘athari ya matamshi tu’ bali ni mbadala wa “juza” na “julisha.” Liko katika lahaja ya Kimvita ( na latumika mpaka hivi leo), na nafikiri liko katika Kipemba na Kimtang’ata pia.
Ni “tanzia” au “taazia”?
Chembelecho (au chambilecho, au chambacho) msemo wa Kiswahili, “Kipya kinyemi, kingawa kidonda.” Ni dasturi ya baadhi ya watu kuvutiwa na kipya kitokacho kwengine, hata kama tangu hapo wanacho chao wenyewe kifananacho na hicho cha kigeni. Hili swala la maneno kama “mubashara” lina tanzu mbili. Utanzu wa kwanza ni huo wa kupenda kukimbilia maneno ya kigeni, hata kama tunayo yetu wenyewe yenye maana hiyo hiyo. Kama ilivyokwisha elezwa, kabla ya habari “mubashara” tumekuwa tukisema habari/ ripoti za moja kwa moja, au za papo kwa papo (wala si “papo” pekee).
Ni “kiasi cha…” sio “kiasi ya…”
Kwa uchache wa nifahamuvyo, lugha fasaha ni kusema “kiasi cha…”, basi haidhuru iwe ni kwa watu au kwa vitu. Yaani, kiasi cha watu kumi, au kiasi cha miti kumi. Kama ambavyo twasema, kitabu cha…, kisa cha…, kiatu cha…, kitambo cha…, na kadhalika, wala hatusemi kitabu ya…, kisa ya…, kiatu ya…, wala kitambo ya… Na ni hivyo kwa sababu maneno yote hayo yamo katika ngeli ya KI/VI. Basi ikiwa kwa maneno hayo niliyoyatolea mfano hatuyatumilii “ya”, kwa nini iwe kwa neno “kiasi”?