Maana nne za “Likikupata, patana nalo”

Karibuni nilikuwa kwenye ziara kwenye mataifa mawili ya Kiarabu – Oman iliyo Ghuba na Morocco iliyo Afrika Kaskazini – ambayo yana tafauti nyingi baina yao, lakini pia yana mfanano mkubwa kwenye mtazamo wao kuelekea lugha ya Kiarabu. Watu wa mataifa yote mawili watakuambia sentensi moja inayofanana: “Kiarabu ni lugha kongwe na ya kihisabati!” Continue reading “Maana nne za “Likikupata, patana nalo””

Vita baina ya ukale na usasa kwenye ‘Kitumbua Kimeingia Mchanga’

Kitumbua Kimeingia Mchanga ni tamthilia ya kimageuzi iliyoandikwa na Said Ahmed Mohamed na kuchapishwa na Oxford University Press East Africa Ltd inayojaribu kuonesha mgongano uliopo kati ya ukale na usasa katika jamii, ambapo mpishano wa kimawazo na kimtazamo baina ya wazee na vijana unayaumba na kuyaumbua mahusiano yao ya siku kwa siku tangu kwenye mambo makubwa na hadi kwenye madogo. Continue reading “Vita baina ya ukale na usasa kwenye ‘Kitumbua Kimeingia Mchanga’”

‘Babu Alipofufuka’, riwaya inayoakisi uhalisia

Riwaya ya ‘Babu Alipofufuka’ imeandikwa na mwandishi maarufu wa kazi za fasihi na mtaalamu wa lugha ya Kiswahili, Profesa Said Ahmed Mohammed, na kuchapishwa na Jomo Kenyatta Foundation mwaka 2001. Katika gamba lake la mbele, pameandikwa: “pengine ni riwaya ya ujasiri mno kupita zote Said A. Mohammed alizowaji kuandika.” Na hivyo hasa ndivyo ilivyo – hii ni riwaya ya kijasiri, ya kimapinduzi. Continue reading “‘Babu Alipofufuka’, riwaya inayoakisi uhalisia”

Puma: Alama ya sanaa katika kuponya majeraha ya kihistoria

Pale hadithi mbili zinapokutana njiani – moja ikiikimbia jana yake na nyengine ikiikimbilia kesho yake – panakuwa na fursa ya kujihakiki upya sio tu kama fanani na hadhira, bali pia kama wahusika wa hadithi zenyewe na kama watenda na watendwa wa mifumo yetu ya kisiasa na kijamii.

Continue reading “Puma: Alama ya sanaa katika kuponya majeraha ya kihistoria”

Waandishi wa zama zetu na dhana ya ‘kuiafrikanisha’ fasihi ya Afrika

Boris Boubacar Diop ana msimamo kuwa: “huwezi kuwa wa kimataifa kama huna uthubutu wa kuwa wa kwenu”, lakini Patrick Mudekereza anasema katika maeneo mengi barani Afrika ukweli ni kuwa waandishi wanafikiri kwa lugha za kigeni kukiwemo kwao, Kongo, na Nuruddin Farah anasema kilichomfanya kuelekea kwenye uandishi wa Kiingereza ni kuwa lugha yake ya Kisomali haikuwa na hati za maandishi yake yenyewe. Continue reading “Waandishi wa zama zetu na dhana ya ‘kuiafrikanisha’ fasihi ya Afrika”

Ushairi: Hisabati zinazotumia maneno badala ya nambari

Ushairi ni sanaa kongwe na pevu. Ni kongwe kwa kuwa ndiyo njia ya kwanza aliyoitumia mwanaadamu kuelezea hisia zake kupitia lugha na sauti hata kabla hajaanza kutumia njia nyengine za kujieleza. Ni pevu kwa kuwa ni bahari iliyobeba kiwango cha juu cha maarifa. Continue reading “Ushairi: Hisabati zinazotumia maneno badala ya nambari”